Mbwana Samatta aipeleka Genk hatua ya Makundi Europa League


Hatimaye Mbwana Samatta ameweza kuandika ukurasa mpya katika historia ya soka lake baada ya kuisaidia timu yake ya Genk kuibuka na ushindi wa bao  2 – 0 dhidi ya NK Lokomotiva ya Croatia .

Ukijumlisha mechi ya kwanza ambayo timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana goli 2 – 2 , basi  kwa Ushindi wa leo  , Genk inasonga mbele kwa jumla ya goli 4 – 2 huku ikiungana  na timu 47 nyingine katika draw ya hatua ya makundi ya Europa League ambayo inategemewa kuchezeshwa hapo kesho usiku .

Mbwana-Samatta-KRC-Genk

Kocha wa Genk , Peter Maes alikianzisha kikosi cha ushindi wa goli 3 – 0  kilichoshinda wikiendi iliyosiha . Mbwana Samatta alikua wa kwanza kufungua hesabu ya magoli dakika ya kwanza  ya mchezo akimalizia pasi ya Mjamaica, Leon Bailey. . Kipindi cha kwanza hakikua na mishemishe nyingi ukiachana na goli la samatta .

Mbwana-Samatta-KRC-Genk-3

Kipindi cha Pili , Genk waliongeza bao la pili dakika ya 50 baada ya Leon Bailey kujitengenezea bao zuri akipiga chenga mabeki wa NK Lokomotiva hadi kupachika mpira wavuni .

Mbwana-Samatta-Genk-Bongosoka

 Genk inarudi tena kwenye hatua ya makundi baada ya miaka mitatu . Bongosoka punde tutakuletea yote unayopaswa kuyajua kuhusu draw ya kupanga makundi ya Europa League inayotegemewa kufanyika masaa kadhaa yajayo…

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com