Mbwana Samatta aizungumzia Hat-trick yake


Baada ya kufunga Hat-trick yake ya kwanza dhidi ya Brondby IF katika mchezo wa kuwania kucheza Europa League msimu wa 2018/19 hatua ya makundi, Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania , Mbwana Samatta amewakosha mashabiki wake baada ya kuweza kutupia Hat-trick yake ya pili kwenye mchezo dhidi ya Zulte Waregem.

“Kwangu ni furaha na ndio kazi yangu, nitaendelea kupambna uwanjani kusaidiana na wenzangu kuisaidia timu kufanya vema,” alikaririwa akisema Samatta  .

Mabao hayo ya Samatta juzi aliyafunga katika dakika ya 31, 67 na 86, huku bao jingine la timu hiyo ambalo lilikuwa la kwanza kwenye mchezo huo likifungwa na kiungo wa Mhispania Alejandro Melero.

Samatta anatarajiwa kuja kujiunga na timu ya Taifa Stars baadaye mwezi huu kwa ajilli ya michezo miwili ya kufuzu kwa fainali za Afrika dhidi ya Cape Verde.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Bonyeza hapa kupata offer kabampe. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com