Mbwana Samatta akaribia kutua Aston Villa , kuandika historia…


Klabu ya Aston Villa inasemekana kua katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa Mshambuliaji wa klabu ya Genk , Mbwana Samatta kwa uhamisho wa paundi milioni 10 sawa na Bilioni 30 za Kitanzania .

Kocha wa Aston Villa , Dean Smith inasemekana anataka kuimarisha safu yake ya ushambuliaji baada ya mshambuliaji wake mbrazil , Wesley kuumia huku akitegemewa kukaa nje hadi mwisho wa msimu baada ya kupata jeraha la goti kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Burnley siku ya mwisho wa mwaka jana .

Samatta, ambaye aliwatungua klabu ya Liverpool kwenye msimu huu wa ligi ya mabingwa ulaya ndio chaguo namba moja la Aston Villa kwasasa .

Samatta mwenye umri wa miaka 27 anahitaji kupata kibali ili aweze kuanza maisha mapya ya soka uingereza na anatarajia kuukosa mchezo dhidi ya Brighton siku ya jumamosi .

Kibali cha kufanya kazi uingereza inawezekana pia kua changamoto kwa Samatta kutokana na Tanzania kuwa nafasi ya 134 kisoka duniani kwa ngazi ya Fifa , kwahiyo Aston Villa inabidi wapeleke ombi maalumu .

Kama Samatta atakamilisha usajili huu atakua ni mchezaji wa kwanza Mtanzania kucheza katika Ligi ya Uingereza .

Tayari Aston Villa wameshakubali kumuachia mshambuliaji wake raia wa Ivory Coast , Jonathan Kodija huku klabu ya Nottingham Forest na Amiens zikionesha nia ya kumsajili .

Kwasasa Aston Villa inashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza baada ya kucheza michezo 22.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com