Mbwana Samatta atajwa kwenda Crystal Palace…


Klabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza ipo katika mchakato wa kuleta mshambuliaji mmoja au wawili kutokana na hali mbaya waliyonayo katika safu ya ushambuliaji .

Kupitia mtandao wa footballfancast  , asilimia 80 ya mashabiki wa Crystal Palace wamesema wanamuhitaji Mbwana Samatta asajiliwe ili kuongeza nguvu katika safu hiyo ya ushambuliaji .

Kwasasa , Mbwana Samatta ndio anayeongoza kwa ufungaji kwenye ligi kuu nchini ubelgiji na usajili kwenda Crystal palace kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi January kitawakosha mashabiki wa timu hiyo wenye kiu ya kuona safu ya ushambuliaji inakaa sawa .

Katika mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Chelsea , Crystal Palace hawakuweza kupiga hata shuti moja golini hali inayoweza kumfanya kocha wao , Roy Hodson kuanza kusaka makali mapya .

Kwa msimu huu Samatta anajumla ya magoli 18 , huku 15 akifunga kwenye ligi kuu na ma 3 kwenye kombe la Europa League .

Ukiachana na Samatta , mshambuliaji wa Liverpool , Dominic Solanke inaelezwa tayari anaelekea kumwaga wino katika Klabu hiyo .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com