Mbwana Samatta kuanza Europa League leo…


Nahodha wa Taifa stars anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji , Mbwana  Samatta leo anaianza safari yake ya hatua ya Makundi katika michuano ya Europa League katika mchezo wa kwanza wa Kundi F dhidi ya wenyeji, Rapid Viena nchini Austria.

katika mchezo mwingine wa kundi hilo,  Sassuolo ya Italia watakuwa wenyeji wa Athletic Bilbao ya Hispania Uwanja wa Citta del Tricolore.

Mbwana-Samatta-Genk-Bongosoka-3

Kumbuka , Genk ilifungwa  bao 2-0 na Standard Liege katika Ligi ya Ubelgiji Jumapili  iliyopita , mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege .

Tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 24 za mashindano yote, 18 msimu uliopita na sita msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com