Mfahamu kocha mpya Simba SC


Muda mchache uliopita , mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wekundu wa Msimbazi , Simba imemtambulisha kocha wake mpya Mbelgiji Sven Ludwig Vandenbroeck .

Vandenbroeck anajiunga na Simba baada ya kutimuliwa kwa Patrick Aussems , kocha aliyeiongoza klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufuzu kucheza robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita.

Sven Ludwig Vandenbroeck  alizaliwa Tarehe 22 September mwaka 1979 huku kibarua chake cha hivi karibuni kikiwa kuifundisha timu ya taifa ya Zambia (February 2016 hadi February 2018) ambapo kibarua chake kiliota nyasi baada ya kushindwa kuipeleka Zambia kwenye michuano ya Mataifa ya Africa , AFCON 2019 .

Sven Mwenye umri wa miaka 40 , aliifundisha pia Cameroon kuanzia July 2018 hadi March 2018 lakini pia kabla ya hapo alishinda ubingwa wa Afrika AFCON mwaka 2017 nchini Gabon akiwa kama kocha msaidizi katika timu ya Taifa ya Cameroon .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com