Micho : Simba imemkosea Heshima Juuko Murshid


Kocha wa timu ya Taifa ya Uganda, Milutin Srejedovic ‘Micho’ amekaririwa na gazeti pendwa la mwanaspoti akisema kua kitendo cha Simba kumsugulisha Benchi Beki wake Juuko Murshid ni kumkosea heshima na kama akiendelea kusugua benchi atahakikisha anamchomoa Klabuni Hapo .

Juuko ambae aliisaidia timu ya Taifa ya Uganda , The Cranes kufuzu  kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani nchini Gabon baada ya miaka 38, ameanza msimu huu wa ligi kuu akichezea Benchi .

Micho aliongezea kwa kusema kua ni jambo la kushangaza kuona mchezaji wa kiwango cha juu kama Juuko anakaa benchi Simba wakati ameisaidia timu yake kufuzu Afcon tena baada ya miaka mingi.

Juuko-Murshid-simba-Bongosoka

“Siwezi kuwaingilia Simba katika masuala yao ya kiufundi lakini kwangu mchezaji kama Juuko kuwekwa benchi ni kumkosea heshima, nimesikia kwamba hajaanza katika mechi yoyote msimu huu, ni jambo la ajabu sana,” alisema Micho .

“Siwezi kukubali katika dakika hizi za lala salama mtu kama Juuko aanze kupoteza hali ya kujiamini, natazama namna ya kumtafutia njia nyingine ya kupata muda wa kucheza hata ikiwezekana kumwondoa hapo Simba,” alifafanua.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com