Mkwasa atangazwa rasmi kuwa kocha mkuu Taifa Stars, Kulamba milioni 28 kwa mwezi !!


“Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi  (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” , Hayo ni baadhi ya maneno ya Rais wa shirikisho la soka Tanzania , Jamal Malinzi alipokua akimtangaza rasmi  Charles Boniface Mkwasa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa , Taifa Stars kwa kipindi cha miezi mitatu wakati Taifa Stars ikipigania kushiriki  kufuzu  mashindano ya  CHAN na AFCON.

Charles-Boniface-Mkwasa-Kocha-Mkuu-Taifa-Stars-bongosoka

Mkwasa ambaye ni Kocha Msaidizi wa Yanga  ametagazwa kuwa kocha wa Stars leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika jijini Dar es Salaam. Jamal  Malinzi  pia amemtangaza kocha Hemed Morocco kuwa msaidizi wa mkwasa. Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha  hao wazawa wamekizi.

Uteuzi huo wa Mkwasa kua kocha mkuu wa Taifa Stars kunamfanya achukue mshahara wa kocha aliyefukuzwa  mwishoni mwa wiki baada ya Taifa Stars kufungwa mabao 3-0 na Uganda Uwanja wa Amaan, Zanzibar , Maart Nooij ambaye alikua anakula dola 12,500 (Kwa sasa ni milioni 28 hivi) kwa mwezi. Je, unafikiri huu ni mwanzo mpya kwa Stars ?

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com