Baba asema mrembo huyu anamkosesha Manyika Jr namba Simba..


“Tatizo kwetu mbagala , hapa nyumba mbele jalalaaa… ” , basi kama wewe unamkumbuka yule mrembo ambae mwishoni kabisa mwa hii video alionekana akija kumchukua Diamond Platnumz , basi huyu ndio mrembo anayetoka na golikipa wa Simba , Manyika Jr ambaye baba yake mzazi Manyika Peter  ameonekana kutopendezwa naye kutokana na mwanaye kuendekeza sana mapenzi na starehe .

BAADA ya kuona kipaji cha mwanae kikipotea wakati akiwa na kazi kubwa ya kulitumikia taifa lake, Baba mzazi huyu  aliibuka na  kumkoromea mwanae.

Manyika mkubwa anasema mwanae ni kama anakula mshahara wa bure Msimbazi kwa sababu ya kushindwa kuitumikia timu hiyo iliyomsajili ikiwa na matumaini naye makubwa kwa uwezo mkubwa wa kisoka aliokuwa nao.

Baba mzazi huyo alisema kinachomponza mwanae ni kukosa nidhamu na pia kutekwa na kuyaendea kasi mahusiano ya kimapenzi aliyonayo kwa sasa. Akizungumza kwa uchungu, nyota huyo wa zamani wa Sigara, Mtibwa Sugar, Yanga na Taifa Stars, alisema mwanaye anapotea kwa sababu ya kuendekeza starehe na huwa anajisikia vibaya anaposikia akiwajibu mbovu waanahabari na hata viongozi  wake kuhusiana na sakata lake la mambo ya mapenzi.

MAnyika-Jr-mchumba-demu-wake-bongosoka-4

Baba Manyika alisema hawezi kuulaumu uongozi wa Simba kwa kitendo cha mwanae kuozea benchini kwani, kijana wake amejisahau na amekuwa akijaribu kumweka kwenye mstari bila mafanikio, jambo linalomuuma kama mzazi.

“Amesajiliwa Simba afanye kazi  siyo kula mshahara wa bure na kuishia kukaa benchi, viongozi hawana tatizo kama angekuwa msaada angepangwa lakini yeye ajiulize na hayo mahusiano aliyonayo kama yanamsaidia katika kazi yake?” Alihoji bila kumuweka hadharani binti huyo anayemzingua Manyika.

“Akipata jibu na atarudi kwenye mstari, kama mzazi najisikia uchungu sana kwa yale anayoyafanya mtoto wangu kwa sababu najua maisha ni nini lakini yeye anaona mjanja ila nina shaka hapo mbele asije akaumizwa vibaya,” alisema Manyika Mkubwa.

Manyika alifunguka zaidi kwa kudai; “Nimecheza nafasi kama yake kwa mafanikio makubwa, ndiyo maana nasema kwa uchungu kwamba jibu ni mwanangu wala siyo viongozi yeye ndiye chanzo kwa sababu wasingeweza kutupa pesa yao bure kumsajili kwa mkataba wa miaka mitatu kama pambo bali kwa ajili ya kufanya kazi yao.”

Alifafanua kuwa hawezi kumkataza mwanae kuendelea na mapenzi na mwanamke aliyenaye, isipokuwa ni vema kuangalia mustakabali wake kwa sababu mtaji wake ni kipaji cha soka na akizembea atakuja kujuta mbeleni.

“Kipindi nilichokuwa nacheza na staa katika jamii nilifuatwa na wanawake wa kila aina na wengine kutaka wagharamikie kwa kila hali lakini nilikuwa na msimamo na kupuuza mambo yao na sitaki mwanangu aangamie,” alisema Manyika Mkubwa.

Kipa Manyika aliposakwa kwa njia ya simu, hakupokea simu aliyopigiwa, lakini kocha wa makipa wa Simba Adam Abdallah, alisema kinachofanya Manyika Jr, asugue benchi ni kutokana na kukosa nafasi mbele ya Vincent Angban aliyepo juu kwa sasa lakini mchezaji huyo si mbaya.
Source: Mwanaspoti

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com