Mshahara wa Abdi Banda Afrika Kusini huu hapa….


Aliyekua beki wa klabu ya wekundu wa Msimbazi , Simba , Abdi Banda ameamua kuweka wazi mpunga atakaokua anapata baada ya kumaliza mkataba wake Simba na kujiunga na klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini .

Banda amefunguka wazi wazi na kusema kuwa klabu ya Baroka FC imekubali kuingia nae mkataba wenye thamani ya  Sh 250 milioni za kitanzania kwa  miaka mitatu.

Mwanzoni mwa wiki hii , Abdi Banda aliingia kwenye mzozo na klabu ya Simba baada ya kufuatilia barua yake ya uthibitisho wa kumaliza mkataba wake lakini  Simba  waligoma kumpa barua hiyo kwa madai kwamba anatakiwa kuandika pia barua ya kuomba jambo ambalo aliligomea.

Baada ya Simba kugoma kumpa Banda barua , aliamua kwenda Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuomba nakala ya mkataba wake ambapo alipatiwa na kuwatumia mabosi wake wapya ambao nao walimwambia aachane na barua hiyo kwani mkataba pekee unaoonyesha umemalizika Mei 30 unatosha.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com