Mshambuliaji mpya Yanga kutua leo


MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga kutoka FC Platinum ya Zimbabwe, Walter Musona anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam leo alasiri kwa ajili ya mazungumzo ya kuichezea timu hiyo.

Musona anayeelezwa kuwa pacha wa Donald Ngoma ndiye aliyefunga bao pekee la FC Platinum kwa mpira wa adhabu ndogo wakati Yanga ilipoifunga Platinum kwa mabao 5-1 kwenye Kombe la Shirikisho la Soka la Afrika (CAF CC) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwaka jana.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika kutoka Yanga, tayari masuala muhimu kuhusiana na ujio wake yamekamilika na kwamba kuna matarajio makubwa wakamalizana kuhusiana na kuichezea Yanga msimu ujao.

Walter-Musona-bongosoka-yanga

“Atafika Dar es Salaam kesho (leo), tunaamini suala lake litaisha na atakuwa mchezaji wa Yanga,” kilisema chanzo hicho. Mtoa habari huyo alisema nyota wawili wa Yanga kutoka Zimbabwe, Ngoma na Thabani Kamusoko, wako nyuma ya mpango wa kumleta Musona kwenye timu hiyo na wamepata baraka kwa uongozi na benchi la ufundi chini ya kocha Hans Pluijm.

“Musona anaweza kucheza nafasi ya namba 10, 8 na 6, lakini pia anaweza kucheza winga zote, ana uwezo mkubwa wa kukaba na kufanya mashambulizi,” kilisema chanzo chetu.

Hata alipoulizwa jana kuhusiana na suala hilo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga alisema atafutwe baada ya saa moja na alipotafutwa baadaye simu yake ilikuwa haipokelewi.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com