Mtanzania kucheza na Ibrahimovic Marekani


Mlinzi wa zamani wa  Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amejiunga rasmi na klabu ya LA Galaxy ya Marekani ambaye nahodha wake kwasasa ni Zlatan Ibrahimovic aliyewahi kuzichezea klabu maarufu za Manchester United , PSG , Barcelona , Inter Milan , AC Milan na Juventus .

Ninja anajiunga LA Galaxy kwa mkopo baada ya kusainiwa mkataba wa miaka minne na klabu ya MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech na timu hiyo kumtoa kwa mkopo kwenda kukipiga LA Galaxy .

MFK Vyskov walimsajili Ninja kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika na Yanga .

Ninja anaungana na kiungo wa kimataifa wa Tanzania , Ally Ng’azi anayekipiga timu ya Minnesota United ya nchini Marekani .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com