Mzimbabwe na Mghana wafuzu vipimo Yanga…


KIUNGO chipukizi wa Ghana, Joseph Tetteh Zutah na mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma  wamefuzu vipimo vya afya walivyofanyiwa katika Hospitali ya Msasani Peninsula chini ya Dk. Humera Gajiyani ambaye aliwapima uwezo wa mapafu yao kufanya kazi, vipimo vya moyo na vipimo vya damu. Pia walienda kwa Dk. Gilbert Kigadyi ambapo walipimwa viungo vyao na wote walionekana hawana tatizo.Hivi sasa wanasubiri  kusaini mkataba wa kuichezea timu ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Ngoma na Zutah waliwasili nchini tayari kujiunga na Yanga iliyopania kuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao. Daktari wa Yanga, Juma Sufiani, amesema kuwa zoezi hilo limekwenda vizuri na muda wowote , wachezaji hao walitarajiwa kusaini mikataba ya kuichezea Yanga msimu ujao.“Tumewafanyia vipimo vya afya na mambo yanakwenda vizuri, hakuna tatizo, lakini siwezi kusema lolote hivi sasa, tusubiri ripoti ya madaktari wenzangu waliopewa dhamana ya kuwafanyia vipimo,” alisema Sufiani.
Donald-Ngoma-na-Joseph-Zutah--wafuzu-vipimo-Yanga-bongosoka

Zutah aliyezaliwa Agosti 22, mwaka 1994 anatokea klabu ya Medeama , wakati Ngoma anatokea FC Platinum. Yanga SC iliitoa Platinum katika hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu, lakini kocha Mholanzi Hans van der Pluijm akavutiwa mno na Ngoma, aliyecheza mechi moja tu ya Zimbabwe baada ya kukosa mechi ya Dar es Salaam kwa sababu alikuwa majeruhi. Na Pluijm ambaye amewahi kufundisha Ghana, ndiye aliyempendekeza Zutah ambaye uongozi wa Yanga SC haujawahi kumuona kabisa, lakini vyanzo vinasema huyo ni mchezaji mzuri anayeweza kucheza pia kama beki wa kulia.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com