Mzimbambwe wa Yanga atua rasmi Jangwani..


NAHODHA wa FC Platinum ya Zimbabwe kiungo, Thabani Kamusoko (pichani) amewasili Dar es Salaam jana  jioni  ajili ya kusaini Mkataba wa kujiunga na Yanga SC.  Kamusoko amepokewa na Meneja wa Yanga SC, Hafidh Saleh jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na moja kwa moja kupelekwa kwenye kikao na viongozi. Kamusako aliyewahi pia kuchezea Dyanamos FC ya Zimbabwe anatarajiwa kusaini Mkataba wa miwili Yanga SC.  Rasta huyo aliyeivutia Yanga SC ilipokutana na klabu yake, FC Platinum katika Kombe la Shirikisho mwanzoni mwa mwaka huu, anatarajiwa kuchukua nafasi ya Kpah Sherman aliyeuzwa Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini. Lakini pia, Yanga SC inafikiria kuwaacha wachezaji wake wengine wawili wa kigeni, beki Mghana Joseph Tetteh Zutah na kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho. Dirisha la usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara linatarajiwa kufungwa leo saa 6:00 usiku  na kutakuwa na nafasi ya kusajili wa wachezaji huru tu kwa wiki moja ya mwisho kabla ya kuanza msimu mpya.

NAHODHA-wa-FC-Platinum-ya-Zimbabwe-kiungo,-Thabani-Kamusoko-Yanga-bongosoka

Baada ya Yanga SC kutolewa katika Robo Fainali michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame imekitathmini kikosi chake na kugundua Zuttah na Coutinho hawana faida. Coutinho alijiunga na Yanga SC msimu uliopita akiletwa na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazil mwenzake, Marcio Maximo na hadi sasa ameichezea timu hiyo mechi 33 na kuifungia mabao sita. Mbrazil huyo alikuwa ana wakati mzuri chini ya kocha Maximo, lakini tangu ujio wa Mholanzi, Hans van der Pluijm amepoteza nafasi katika kikosi cha kwanza.
Zuttah amesajiliwa Juni mwaka huu kufuatia kupendekezwa na kocha Pluijm, lakini baada ya wiki mbili za Kombe la Kagame, uongozi umeona hana umuhimu.
Mbali na Sherman, Coutinho na Zuttah wachezaji wengine wa kigeni Yanga SC ni Mkongo, Mbuyu Twite, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com