Ndanda FC VS Simba hapatoshi leo Mtwara , takwimu hizi hapa….


Ligi kuu ya vodacom inaendelea leo huku michezo mitatu ikipigwa leo . Mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka hii leo ni kati ya Ndanda FC na Simba utakaopigwa katika dimba la Nangwanda Sijaona , Mtwara .

Mchezo huu unasubiriwa hasa baada ya Simba kuvuliwa ubingwa wa kombe la FA na Green Warriors pamoja na kumtimua kocha wake , Joseph Omog ambaye tayari ameshaondoka nchini .

Kocha msaidizi raia wa Burundi , Masoud Djuma  ambaye amepewa mikoba ya Omog kwasasa atakua na kazi ya zaida leo ambapo Ndanda FC watatambulisha vifaa vyao vitatu walivyosajili kipindi cha dirisha dogo la usajli akiwemo kiungo Mrisho Ngasa aliyemalizana na Mbeya City , Mshambuliaji Ame Ali aliyekua Kagera Sugar na kiungo Salim Telela .

Ndanda FC ambao wanashikilia nafasi ya 11 , wakiwa na pointi 11 huku wakicheza michezo 11 wanahitaji ushindi leo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kukwepa kushuka daraja .

Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 23 , nyuma ya Azam FC ambayo inaongoza ligi ikiwa ishacheza michezo 12 ya ligi .

Kocha msaidizi wa Simba , Masoud Juma amesema hana wasiwasi wowote na mikoba aliyoachiwa na kwakuwa ana uzoefu na ligi za Afrika Mashariki na atagemea kupata ushindi kwenye mchezo wa leo .

“Nilikua kocha mkuu huko nilipotoka . Kuwa kocha mkuu wa muda kwa simba sio kitu kipya kwangu . Nipo tayari kupambana na changamoto za ligi na amini , tutakuja na matokeo mazuri zaidi”  .

Je , takwimu zinasemaje ? Simba na Ndanda FC zimekutana mara  6 tokea Ndanda FC ipande daraja mwaka 2014 . Katika michezo yote timu hizi zilipokutana , Simba ina rekodi nzuri ya  kushinda mechi zote 6 huku ikiwa na jumla ya goli 15 na ndanda goli 1 katika mechi zote za misimu mitatu iliyopita . Kwa takwimu hizi , Simba inategemea kuingia uwanjani leo ikiwa na matumaini makubwa ya kuondoka na pointi 3 .

Michezo mingine ya leo inategemewa kuwaona Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Majimaji ya Ruvuma  katika uwanja wa Manungu Complex . Lipuli FC inategemewa kuwakaribisha Prisons ya Mbeya kwenye mchezo utakaopigwa  katika uwanja wa Samora , Iringa .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com