Ngorongoro Heroes kumenyana na DRC Congo leo taifa…


Timu ya taifa ya vijana wenye chini ya umri wa miaka 20 , Ngorongoro Heroes leo wanatarajiwa kuvaana na Timu ya vijana wa DRC Congo  kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya Fainali za Vijana chini ya umri wa miaka 20, (AFCON)  zitakazofanyika mwakani nchini Niger . Mchezo wa leo unatarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni katika  Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam .

Kocha wa Ngorongoro Heroes , Ammy Ninje amewahimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia vijana wake wa wakitoa dozi kwa wenzao wa DR Congo katika mechi ya kuwania fainali za Afrika.

Naye Kocha wa DR Congo, Jean Claude Mukanya, alisema wanaamini mchezo huu utakuwa mzuri kwao baada ya kuwa na vijana wanaocheza ligi za nje.

Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa tarehe 22 Aprili katika uwanja wa  Complexe Omnisports Stade des Martyrs jijini Kinshasa.

Ngorongoro Heroes  itaingia kwenye mchezo wa leo ikitoka kushinda mechi mbili za kujipima dhidi ya Morocco 1-0 na Msumbiji 2-1.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Bonyeza hapa kupata offer kabampe. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com