Ni Simba VS Yanga leo kuwania Ngao ya jamii….


Klabu za  Simba na Yanga zitakua na kibarua kizito leo jioni pale zitakapokutana katika mchezo wa  wa Ngao ya Jamii utakaopigwa uwanja wa Taifa , Dar-es-salaam majira ya saa 10 jioni . Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa ni Februari mwaka huu, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 .

Timu zote mbili zilipiga kambi Visiwani Zanzibar, zikijiandaa na mchezo huo maalumu na kila timu imeweza kucheza mechi za kirafiki kuvipima vikosi vyao kabla ya mchezo huo.

Yanga wamecheza mechi nne mbili Dar es Salaam na mbili Zanzibar ambapo kati ya hizo imeshinda tatu na kupoteza moja wakati Simba imecheza mechi sita imeshinda tatu imetoka sare mbili na kufungwa mchezo mmoja.

Kwa tathimini ukiangalia viwango vya timu zote mbili Simba licha ya kusajili wachezaji wenye majina makubwa, lakini timu yao imeonakana kuwa na mapungufu kwenye umaliziaji kwani katika mechi sita walizocheza wameweza kufunga mabao nane . mchezo wa mwisho dhidi ya Gulioni wakifunga mabao matano tofauti na mechi nyingi tano ambazo walikuwa wakipata ushindi hafifu wa bao 1-0.

Yanga wao katika mechi yao ya kwanza ya kirafiki waliifunga Moro Kids mabao 5-0, kisha wakaifunga Singida United mabao 3-2, na baadaye wakafungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting. Walipokwenda Zanzibar wakaifunga Mlandege mabao 2-0 kabla ya kumaliza na Jamhuri ambayo waliifunga bao 1-0.

Kocha George Lwandamina ataendelea kuwategemea Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Ibrahim Ajibu, Thabani Kamusoko na Papy Kabamba Tshishimbina, kipa Youth Rostand ambao wapo fiti kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.

Kocha wa Simba Joseph Omog mtaalam wa mfumo wa 4-4-2 niwazi ataingia kwenye mchezo huo akiwa na hamu ya kutaka kupata ushindi ili kuwadhihirishia mashabiki wake kile ambacho amekuwa akikiwaza nacho ni ubingwa.

Katika mechi 98  za Ligi Kuu na iliyokuwa Ligi Kuu ya Muungano zilizozikutanisha timu hizo tangu mchezo wa kwanza Juni 7, mwaka 1975, Yanga imeshinda mara 36 wakati Simba imeshinda mara 26 na mechi nyingine 33 timu hizo zikitoka sare.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com