No mashabiki Bongo, wachezaji kupimwa Corona…


Kikao cha kamati ya uongozi chini ya shirikisho la soka nchini Tanzania, TFF kimetoa maadhimio yake hii leo, juu ya mwenendo mzima wa ligi endapo itarejea baada ya siku 30 zijazo, kama ilivyoamuliwa na serikali ikiwa ni njia ya kuepusha usambaaji wa virusi vya ugonjwa wa Corona.

Kikao cha kamati ya uongozi cha TFF kimeazimia kuwa, baada ya siku 30 serikali itakaporuhusu michezo kuendelea, mechi za ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili na ligi ya mabingwa wa mikoa zitachezwa bila watazamaji/mashabiki, ili kudhibiti kusambaaa kwa virusi vya Corona.

Taarifa hiyo leo imetolea na mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo mara baada ya kikao ambacho kimehudhuriwa pia na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Wachezaji wote kupimwa Corona…

Katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira salama zaidi katika ligi, kikao hicho pia kimefikia makubaliano ya kuwafanyia vipimo wachezaji wote wanaoshiriki ligi husika, pindi zitakaporejea tena. Vipimo hivyo vya Corona vitafanywa ili kubaini endapo kuna maambukizi yoyote ya kudhibitiwa kabla ya kuanza kwa ligi husika.

” kikao kimeazimia kwamba pale ambapo serikali itakuwa imeridhia ligi kuendelea, basi wale wachezaji wote husika wa hizo ligi wanatakiwa wafanyiwe vipimo…,”aliongeza Kasongo, mwenyekiti wa Bodi ya Ligi.

Maadhimio manne (4) ya kikako cha kamati ya uongozi, TFF..

  1. Kuridhia tamko la serikali kuhusu usimamishwaji wa mashindano yote yaliyo chini ya TFF.
  2. Kuwapima Corona, wachezaji wote wa mashindano/ligi husika pindi ligi itakaporejea.
  3. Mechi za ligi zitachezwa bila watazamaji/mashabiki pindi ligi itakaporejea.
  4. Kumaliza ligi ndani ya mwezi sita (6) endapo hali itakuwa shwari.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com