NYOTA wa soka Uingereza wanavyopiga mkwanja wa ajabu…


Ligi kuu ya soka ya England, ni ligi yenye umaarufu mkubwa pengine kuliko ligi yoyote barani Ulaya na duniani, kwa ujumla.

Hii inatokana na mambo mengi sana, ikiwemo uwekezaji mkubwa unaofanywa na shirikisho, vilabu, wamiliki na makampuni mbalimbali ya udhamini. Hali hii huifanya ligi na timu kuwa na vyanzo vingi vya mapato na hivyo kuwa na thamani ya juu zaidi.

Matokeo yake ni kwamba, vilabu havioni shida katika kuwekeza kuwalipa vizuri wachezaji, kwani kufanya vizuri zaidi kwa timu ndiko kunatoa nafasi ya uchumi wa timu husika kuimarika.

Hawa ndio nyota ambao wanafaidika zaidi na uwekezaji huo, kwani wanavuta mkwanja mrefu zaidi kwa wiki kama mshahara, kuliko wachezaji wengine wote ndani ya ligi hiyo.

David De Gea

1. David De Gea – Man Utd

Huyu ndiye mchezaji anayelipwa hela nyingi kuliko wachezaji wote ndani ya ligi kuu ya Uingereza. De Gea anakunja Paundi 375,000 sawa na Shilingi Milioni 996.2 za kitanzania (Tsh) kwa wiki.

Golikipa huyu amelelewa na kukulia katika klabu ya Atletico Madrid ya Hispania na alitimkia Uingereza, kujiunga na Manchester United, mwaka 2011 chini ya kocha Sir Alex Ferguson. De Gea katika umri wa miaka 29 amekuwa msaada mkubwa sana kwa mashetani hao wekundu wa jiji la Manchester.

KDB

2. Kelvin De Bruyne (KDB) – Man City

Huyu ndiye anayefuatia katika orodha hii. KDB amekuwa na msaada mkubwa kwa Man City hasa katika utengenezaji wa mabao, huku akiiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi, mara 2 mfululizo hivi sasa.

KDB anaweka kibindoni paundi 320,833 kwa wiki, sawa na Tsh. Milioni 852.3.

Raheem Sterling

3. Raheem Sterling – Man City

Nyota huyu wa Man City anakuwa mchezaji wa pili wa klabu hiyo kuwepo katika orodha hii. Sterling aliingia City, mwaka 2015 akitokea Liverpool na tangu hapo amekuwa na maisha ya mafanikio katika soka na maisha binafsi pia kulingana na pesa anayoingiza.

Sterling analipwa kiasi cha Paundi 300,000 sawa na Tsh. Milioni 796 kwa wiki.

Paul Pogba

4. Paul Pogba – Man Utd

Kiungo mwenye mbwembwe nyingi ndani na nje ya uwanja. Pogba alikulia Man Utd kabla ya kuondoka kuelekea Juventus na kurejea tena kwa mashetani wekundu akiwa katika kiwango bora zaidi. Msimu huu amecheza mechi saba (7) tu za ligi kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.

Paul Labile Pogba anatia mfukoni kiasi cha Paundi 290,000 sawa na Tsh. Milioni 769 kwa wiki.

Mesut Ozil

5. Mesut Ozil – Arsenal

Kiungo wa kijerumani anayesifika kwa pasi zenye macho, ndiye mchezaji pekee kutoka nje ya timu za jiji la Manchester anayelipwa zaidi. Ozil hajawa na maisha mazuri sana ndani ya Arsenal katika misimu ya karibuni kutokana na kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Mesut Ozil analipwa Paundi 268,750 sawa na Tsh. Milioni 712 kwa wiki.

Wachezaji wengine ni (malipo kwa wiki):

6. Antony Martial (Man Utd) – paundi 250,000 (Tsh. Milioni 663)

7. Sergio Aguero (Man City) – paundi 230,135 (Tsh. Milioni 610)

8. Mohamed Salah (Liverpool) – paundi 200,00 (Tsh. Milioni 530)

9. Harry Kane (Tottenham) ” ”

10. Marcus Rashford (Man Utd) ” ”

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com