Obrey Chirwa awanyolea upara Azam FC


Mshambuliaji  wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa, ameamua kubadili  mwonekano wake kwa  kunyoa nywele zote kichwani huku ikielezwa ni kutoa mikosi ili awafunge wapinzani wao Azam FC.

Yanga na Azam zinatarajiwa kukutana kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Mzambia huyo amekuja na staili hiyo huku akiachia ndevu, muonekano ambao ameanza kuonekana nao kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Rafiki wa Chirwa alikaririwa akisema kua Chirwa  ameipania mechi dhidi ya Azam FC , hivyo amepanga kufanya kila jitihada kuhakikisha anawafunga kisha bao atakalofunga liwe zawadi kwa mtoto wake aliyezaliwa wiki iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram alitupia picha yake akiwa mazoezini akiwa na upara na kuandika ‘new look’.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com