Omog aeleza kwanini anataka kuwafunga Yanga


Wakati  homa ya pambano la watani wa jadi likizidi kuongezea, Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, amesema kuwa mawazo yake yapo kwenye ubingwa na si katika mchezo dhidi ya Yanga utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

Omog ambaye yupo na kikosi chake cha timu hiyo kambini Morogoro, alisema kuwa pamoja na umuhimu wa kutaka kulipa ‘kisasi’, bado kwake suala la kutwaa ubingwa ndiyo analipa kipaumbele.

“Tunataka kuifunga Yanga kwa sababu lengo letu ni ubingwa msimu huu, siifikirii Yanga peke yake, baada ya mchezo wa Jumamosi tuna michezo mingine mingi ambayo nayo ni muhimu pia kwetu kushinda ,” alisema Omog.

Kocha huyo alieleza kwamba ‘ukubwa’ wa mchezo huo upo zaidi kwa mashabiki na wanachama wa timu hizo mbili kongwe hapa Tanzania.

Joseph-Omog-na-Jackson-Mayanja-Simba-Kocha-Bongosoka

“Nafahamu mchezo wa Simba na Yanga unachukua hisia za mashabiki wengi, lakini nataka wachezaji wangu wauchukulie kama michezo mingine tu, lengo letu namba moja nataka liwe ubingwa na sio kuifunga Yanga,” Omog alisema.

Aliongeza kuwa mazoezi wanayofanya sasa ni kwa ajili ya kurekebisha mapungufu ambayo aliyabaini katika mechi iliyopita huku akitaka washambuliaji kuongeza umakini wanapopata nafasi ya kufunga.

“Vipo vitu vidogo vidogo ambavyo navifanyia kazi, tunatengenezan nafasi nyingi lakini umakini sio mkubwa, nataka kulimaliza tatizo hili, baada ya hapo tutaendelea na mazoezi mepesi,” alisema Omog.

Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea Dar es Salaam keshokutwa tayari kwa mchezo huo ambao utakaochezeshwa na rea Martin Saanya atakayesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Samuel Mpenzu wa Arusha.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com