Omog awakemea Mavugo na Ajib kwa uchoyo wa pasi


Wakati kesho klabu ya wekundu wa msimbazi Simba inategemea kuingia uwanjani kumenyana na JKT Ruvu  , Kocha mkuu wa Simba , Joseph Omog ameonekana kukerwa na ubinafsi unaoonyeshwa na Washambuliaji wake , Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib .

Baada ya kuwatazama kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu na zile mbili za kirafiki dhidi ya AFC Leopards na URA  , Omog aligundua  kila mmoja amekuwa akicheza kichoyo anapokuwa uwanjani na mwisho wa siku kuwaweka chini  washambuliaji hao tegemeo na  kuwataka kuacha uchoyo uwanjani na kucheza kwa ajili ya timu na si mafanikio binafsi.

Omog alisema amewaweka chini mastraika hao wawili na kuwapa onyo kali huku akisisitiza kuwa mchezaji ambaye ataendelea na tabia hiyo ya uchoyo atasugua  benchi au kumtoa uwanjani kama akiwa anacheza.

Mavugo-Ajib-Simba-Bongosoka

“Timu kwanza mtu baadaye, hakuna ubinafsi kama mtu anajiona yeye ni mbinafsi aachie ngazi wengine wafanye kazi, hatupo hapa kujionyesha kila mtu anaweza,” alisema Omog.

Alisema kitendo cha mastraika hao wawili kucheza na kunyimana pasi katika mchezo uliopita dhidi ya Ndanda FC kulilipa wakati mgumu benchi la ufundi la timu hiyo katika kipindi chote cha dakika 90 za mchezo huo.

“Tulikuwa tuna uwezo wa kufunga mabao zaidi ya matano siku ile, lakini kwa tabia zao za kunyimana pasi na kucheza kibinafsi kulitupa wakati mgumu sana pamoja na kuwa tulishinda mchezo ule,” alisema Omog.

Aliongeza kusema kuwa Simba msimu huu imedhamiria kufanya kweli ndio maana benchi la ufundi la timu hiyo limeweza kusajili kikosi kipana kilichosheheni lundo la wachezaji wenye vipaji vya hali juu.

“Hakuna Mungu mtu, nina washambuliaji wengi kama Fredrick Blagnon, Danny Lyanga na Ame Ali kwa hiyo atakayeshindwa kwenda na sera zetu aachie ngazi mapema,” alisisitiza Omog.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com