Omog : wapinzani mkae mkao wa kula


Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema hana shaka timu za Ligi Kuu Bara zimesikia salamu zao kutoka Uwanja wa Taifa juzi, na hivyo kuwataka kukaa mkao wa kula.

Simba iliichapa AFC Leopards ya Kenya mabao 4-0 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki katika kuhitimisha tamasha la Simba Day.

Omog alisema kwa kiwango kilichooneshwa katika mechi hiyo kinamfanya aanze kuwaza ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao.

Simba ikicheza kwa mara ya kwanza Uwanja wa Taifa chini ya Omog, kwenye mechi hiyo wachezaji wake wageni Shizza Kichuya na Laudit Mavugo walionesha kiwango cha hali ya juu na kufungua akaunti zao za mabao.

Omog alisema matokeo ya mchezo huo yalikuwa sawa na salamu kuelekea kuanza msimu mpya wa ligi na hivyo vilivyoonekana ni vidogo, kwani bado kuna mambo makubwa ambayo hawakuyaonesha siku hiyo kutokana na kuhofia wapinzani wao kuzisoma mbinu zao.

Joseph-Omog-Kocha-Mkuu-SImba-Bongosoka

“Nafurahi tulicheza kwa kiwango cha juu hasa kipindi cha pili na tulifanya kila tulichotaka kwa sababu tulikuwa bora zaidi ya wapinzani wetu nadhani kwa sasa tupo tayari kwa ligi kwa sababu kile nilichowafundisha vijana wangu nimeona kimepokewa vizuri na kufanyiwa kazi ipasavyo,” alisema Omog.

Mcameroon huyo aliyewahi kuifundisha Azam FC misimu miwili iliyopita, alisema anajivunia kuwa na kikosi kipana chenye wachezaji wengi vijana ambao wana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu kutokana na uwezo waliokuwa nao, jambo ambalo anaamini litakuwa na faida kubwa kwao kwenye ligi ijayo.

Alisema anajua ligi itakuwa ng umu na yenye ushindani mkubwa lakini kwa maandalizi waliyofanya anaamini msimu ujao utakuwa ni wa Simba kwani wanakila sababu ya kupata mafanikio kutokana na usajili waliofanya na malengo yao kuelekea msimu ujao.

Baada ya mchezo huo kikosi cha Simba kiliingia kambini kujiandaa na mchezo wao wa kwanza wa ligi dhidi ya Ndanda FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Agosti 20, mwaka huu.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com