Pata kumfahamu vizuri Ramadhan Singano a.k.a ‘Messi’…


Jina lake halisi anaitwa Ramadhan Yahaya Singano au ukipenda unaweza kumuita “Messi” , japokua yeye mwenyewe hapendi kuitwa hivyo ila tu inabidi akubali kutokana na mashabiki kupenda kiwango chake awapo uwanjani na kukifananisha na kile cha messi wa Barcelona. Alianza kuitwa messi tokea wakati anachezea Simba B .Singano alizaliwa miaka 22 iliyopita katika jiji la Dar es salaam mitaa  ya kurasini. Elimu yake ya msingi aliipata katika shule ya msingi mgulani mwaka 2000 ambapo baada ya wazazi wake kufariki mwaka 2003 ilibidi apelekwe katika shule ya watoto yatima ya Al Farouk iliyopo tabata.

Ramadhan-Singano-messi-simba

Kipaji cha Singano kilianza kuonekana akiwa anachezea timu ya mtaani kwao iliyojulikana kama ubatani  huku alipokua katika shule ya Al Farouk kuna mwalimu alikua akimpeleka Kariakoo kwenye soka la mchangani na huko ndipo alipokuza kipaji chake kwa sana.

Singano alianza kujulikana kama mchezaji  anayeweza kusakata kandanda kiwango cha ligi kuu katika mashindano ya Copa Coca-Cola mwaka 2009 ambapo viongozi wa Simba B wakishuhudia kiwango chake cha hali ya juu. Hivi sasa messi ni mchezaji wa simba japo kuna misuguano ya kimkataba na klabu hiyo na anategemewa kuwa moja ya wachezaji tishio kwenye msimu ujao.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com