Ratiba ya mapinduzi cup 2019 hii hapa..


Michuano ya mapinduzi Cup imeanza kutimua vumbi hapo Jana , Januari Mosi hadi Januari 13, 2019 visiwani Zanzibar, ambapo ratiba yake ikiwa tayari imetolewa huku Simba na Yanga zikiwa katika makundi mawili tofauti .

Timu 6 zitakazoshiriki kutoka Zanzibar ni KVZ, KMKM, Jamhuri, Chipukizi, Mlandege na Malindi huku timu 3 za Azam, Simba na Yanga zikitoka Tanzania Bara.

Katika michuano hiyo ambayo huchezwa mwezi Januari kila mwaka, Kundi A lina timu za Chipukizi, Mandege, KMKM, na Simba, wakati kundi B limesheheni timu za KVZ, Malindi, Jamhuri, Azam na Yanga.

kupitia Kamati ya michuano hiyo ,  zawadi za washindi zimeongezwa ambapo sasa mshindi wa kwanza atakuwa akipata shilingi milioni 15 za Tanzania badala ya milioni 10, na mshindi wa pili ambaye alikuwa anapata milioni 5, sasa atapata milioni 10.

Kundi A : Chipukizi , Mlandege , KMKM , Simba

kundi B : KVZ , Malindi , Jamhuri , Azam , Yanga

TareheMudaUwanjaMechi
01/01/2019Saa 10:15Uwanja wa AmaanKVC VS Malindi (Kundi B)
02/01/2019saa 10:15Uwanja wa AmaanChipukizi VS Mlandege (Kundi A)
02/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanAzam FC VS Jamhuri (Kundi B)
03/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanKVZ  VS Yanga (Kundi B)
04/01/2019saa 10:15Uwanja wa AmaanJamhuri VS Malindi (Kundi B)
04/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanChipukizi  VS Simba (Kundi A)
05/01/2019saa 10:15Uwanja wa AmaanMlandege VS KMKM (Kundi A)
05/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanYanga  VS Azam FC (Kundi B)
06/01/2019saa 10:15Uwanja wa AmaanJamhuri VS KVZ (Kundi B)
06/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanKMKM VS Simba (Kundi A)
07/01/2019saa 10:15Uwanja wa AmaanAzam FC VS KVZ (Kundi B)
07/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanYanga VS Malindi (Kundi B)
08/01/2019saa 10:15Uwanja wa AmaanKMKM VS Chipukizi (Kundi A)
08/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanSimba VS Mlandege (Kundi A)
09/01/2019saa 10:15Uwanja wa AmaanYanga VS Jamhuri (Kundi B)
09/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanAzam FC  VS Malindi  (Kundi B)
10/01/2019Mapumziko
11/01/2019saa 10:15Uwanja wa AmaanNusu Fainali ya kwanza
11/01/2019saa 2:15Uwanja wa AmaanNusu Fainali ya pili
12/01/2019Mapumziko
13/01/2019saa 9:30Uwanja wa GombaniFainali

Kwa mujibu wa kanuni za michuano, endapo Azam fc watachukua kombe hili msimu huu, wataondoka nalo moja kwa moja kwani watakuwa wamechukua mara 3 .

Mashidano yatafanywa katika viwanja vya Amaan (kwa mechi zote mpaka nusu fainali) na Uwanja wa Gombani kwa mechi ya fainali.

Mechi za Amaan zitakuwa zinachezwa saa 10:15 jioni na saa 2:15 usiku huku mechi ya fainali ikitarajiwa kuchezwa saa 9:30 jioni.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com