Ratiba ya raundi ya 16 kombe la FA hii hapa….


SIMBA imepangwa kucheza na Singida United, Yanga na JKT Mlale katika raundi ya 16 ya michuano ya kombe la FA.

Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mechi za raundi hiyo zitachezwa kuanzia Februari 26 mpaka Machi mosi mwaka huu kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Ibrahim-Jeba-Mtibwa-Sugar

“Michuano ilishirikisha timu 64 kutoka Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, inaingia katika mzunguko wa nne huku kukiwa na timu kutoka katika ngazi zote za ligi za TFF, jambo ambalo linamaanisha kuwa kuna ushindani wa kutosha,” alisema Kizuguto.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Februari 26, Ndanda FC watawakaribisha JKT Ruvu katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara, huku Coastal Union wakiwa wenyeji wa wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Februari 27, Mwadui FC watawakaribisha Rhino Rangers kwenye uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga na Tanzania Prisons watacheza na mshindi kati ya Mbeya City/ Wenda FC kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Februari 28, michezo mitatu itachezwa ambapo Simba watawakaribisha Singida United katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Panone FC watacheza dhidi ya Azam FC Uwanja wa Ushirika, Moshi huku Toto African wakicheza na Geita .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com