Rekodi ya John Bocco dhidi ya Simba utaipenda….


Zikiwa zimesalia siku mbili  kabla ya kupambana na Simba, Nahodha wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ anatarajiwa kupambana kuzidisha rekodi yake ya mabao aliyoiweka katika mechi ambazo azam FC imecheza na Simba .

Bocco ndiye mshambuliaji pekee nchini mpaka sasa aliyeweza kuzitesa timu za Simba na Yanga kwa kufunga mabao, kila anapokutana nazo katika mechi mbalimbali.

Ukiondoa rekodi ya kuifunga Yanga jumla ya mabao 12, Bocco mpaka sasa amefanikiwa kutikisa nyavu za Simba mara 18 katika mechi za mashindano mbalimbali.

Bocco ataingia kwenye mchezo wa jumamosi dhidi ya Simba  akiwa na morali kubwa ya kuendeleza rekodi yake ya kufunga kwani katika mechi ya mzunguko wa kwanza msimu uliopita alitupia mawili kwenye sare ya 2-2, huku ya wekundu hao yakifungwa na Ibrahim Ajib.

john-bocco-azam-fc

Akizungumzia rekodi yake hiyo kama ina nafasi, Bocco alisema hawezi kuangalia historia bali anachotaka kukifanya ni yeye kupambana na kufunga mabao katika mchezo huo na hatimaye kuibeba timu yake kuzoa pointi zote tatu.

“Kwa sababu mimi ni mshambuliaji, nikifunga naamini timu yangu itapata pointi tatu, kikubwa kinachonipaga hamasa kwenye mechi hizi kubwa ni wachezaji wenzangu wananipa ushirikiano mzuri na mimi mwenyewe kujituma kwa hiyo najikuta nacheza vizuri na kufunga mabao na kuisaidia timu yangu,” alimalizia.

Simba-VS-Azam-Matokeo Bongosoka 3

Bocco ambaye ni mchezaji pekee mwenye rekodi ya aina yake ndani ya Azam FC, ataingia kwenye mchezo huo akiwa yupo kileleni mwa msimamo wa wafungaji bora msimu huu akiwa na mabao matatu sambamba na wacheaji wengine watatu.

Wengine wanaomfuatia ni Rafael Daud (Mbeya City), Laudit Mavugo (Simba) na Hood Mayanja (African Lyon).

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com