Simba mzigoni leo , mapinduzi cup..


leo klabu ya wekundu wa msimbazi , Simba itashuka dimbani  kucheza na timu  ya Taifa Jang’ombe katika mchezo wa kombe la Mapinduzi, utakaochezwa saa 2:30 usiku leo kwenye Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Simba ambayo inaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara inaratajiwa kuwakosa Fredrick Blagnon ambaye ni mgonjwa, Ibrahim Ajib ambaye yupo kwenye majaribio Misri na Juuko Murshid Juuko ambaye yupo katika maandalizi ya mashindano ya Afrika (AFCON) na timu yake ya taifa ya Uganda.

Hata hivyo kukosekana kwa wachezaji hao hakutaweza kuathiri timu hiyo kwa vile imecheza michezo mitatu bila nyota hao na imeshinda michezo yote.

Kabla ya Simba kucheza, mabingwa watetezi, URA ya Uganda itavaana na KVZ kuanzia saa 10:00 mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkubwa katika kundi A.

Kikosi cha Simba kilichopo Zanzibar kinaongozwa na nahodha Jonas Mkude, mlinda mlango Daniel Agyei, Javier Bukungu, Mohamed Hussein, Abdi Banda, Method Mwanjali, Shiza Kichuya, Mwinyi Kazimoto.

Wengine ni Mzamiru Yassin, James Kotei, Pastory Athanas, Mohamed Ibrahim, Peter Manyika, Hamad Juma, Novatus Lufunga, Juma Luizio, Said Ndemla, Moses Kitandu na Laudit Mavugo.

Mechi za Kundi B zinatarajiwa kuanza kesho kwa Azam FC kumenyana na Zimamoto kuanzia saa 10:00 jioni kabla ya Yanga kumenyana na Jamhuri saa 2:30 usiku.

Yanga itamkosa beki wake raia wa Togo, Vincent Bossou ambaye  anatumikia timu yake ya taifa iliyo kwenye maandalizi ya mwisho ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayotarajiwa kuanza Januari 14 nchini Gabon.

Mashindano ya Mapinduzi ni maalumu kusheherekea sherehe za Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyofanyika Januari 12, 1964 ambayo ilikuwa vita ya dakika 45.

Timu ambazo zimewahi kutwaa kombe la Mapinzuzi toka mwaka 2007 ni Yanga, 2008 Simba, 2009 Miembeni, 2010 Mtibwa Sugar, 2012 -2013 Azam FC , 2014 KCCA ya Uganda, 2015 Simba na 2016 ni URA ya Uganda na msimu huu hatujui litachukuliwa na timu gani.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com