Simba SC waichapa Mtibwa Sugar 1 – 0


Simba SC leo imefanikiwa kukusanya pointi tatu baada  ya kushindwa kufanya hivyo katika michezo minne iliyopita, ambapo mchezo wa mwisho Simba SC kuibuka na pointi tatu ni dhidi ya Coastal union uliochezwa katika uwanja wa Mkwakwani machi 19.

Leo Simba SC walikuwa wageni wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro na Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kikosi-cha-Simba-SC

Katika mchezo wa leo Simba SC walitengeneza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza na kushindwa kuzitumia huku Mtibwa sugar nao wakishindwa kuzitumia nafasi walizotengeneza.

Hali hiyo iliendelea katika kipindi cha pili kabla ya Abdi Banda kutumia nafasi aliyotengenezewa na Mohammed Hussein katika dakika ya 71 na kuipatia Simba SC goli pekee la mchezo huo na kupelekea mchezo kumalizika kwa Simba SC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com