Simba SC yaitandika Ndanda FC , Bocco afanya yake….


Klabu ya wekundu wa Msimbazi , Simba , leo imeweza kuendeleza rekodi yake ya kuifunga klabu ya Ndanda FC katika kila mechi ya ligi kuu waliokutana baada ya leo kuitungua goli 2 bila majimu katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliopigwa katika uwanja wa Nangwanda Sijaona , Mtwara .

Nyota wa mchezo wa leo alikua John Bocco ambae aliweza kutumbukiza nyavuni magoli yote mawili ya Simba . Goli la kwanza alilifungwa kwa kichwa dakika ya 52 baada ya kumalizia mpira mzuri wa kona iliyopigwa na  winga Shiza Kichuya kutoka upande wa kulia.

Dakika 4 baadae Bocco aliweza kuwainua tena mashabiki wa Simba kwa kutupia bao la pili  akitumia  vizuri makosa ya mabeki wa Ndanda na kipa wao, Jeremiah Kisubi kuzembea kuokoa mpira mrefu ulioingizwa kwenye eneo lao la hatari.

Ushindi wa leo wa Simba unazidi kumuongezea imani kocha wao , Masoud Djuma  ambaye katika mchezo wake wa kwanza ameweza kukiongoza kikosi hicho kuondoka na ushindi baada ya aliyekuwa kocha mkuu , Joseph Omog kutimuliwa.

Kwa ushindi wa leo, Simba inafikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 12, sawa na Azam FC walio nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao.

Mabingwa watetezi Yanga SC wenye pointi 21 wanaendelea kushika nafasi ya tatu na wataendelea kukaa hapo hata wakishinda kesho dhidi ya Mbao FC mjini Mwanza sana washuke tu kama watatoa sare au kupoteza na Singida United washinde ugenini dhidi ya Njombe Mji FC.

Katika michezo mingine ya ligi kuu iliyopigwa leo , Tanzania Prisons waliweza kuibuka na ushindi wa goli  1 – 0 dhidi ya wenyeji, Lipuli FC Uwanja wa Samora mjini Iringa. Nao Mtibwa Sugar wameitandika  MajiMaji goli  2-1  katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa  Manungu, Turinia, Morogoro.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com