Simba VS Azam hapatoshi leo ngao ya jamii


Klabu za Simba na Azam FC leo zinaingia dimbani uwanja wa Taifa , Dar-es-salaam kwenye mchezo wa Ngao wa jamii , kuashiria kuanza rasmi kwa msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara .

Timu zote zitaingia uwanjani leo baada ya kutoka katika mechi zao za kimataifa, ugenini, Simba ilicheza na UD Songo nchini Msumbiji na kutoka suluhu, wakati Azam FC walicheza na Fasil Kenema ya Ethiopia na kufungwa bao 1-0.

Azam FC inatarajia kuwakosa nyota wake wawili katika mchezo wa leo ambao ni Agrey Morris na Mudathir Yahya .

Naye mshambuliaji wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere alikaririwa alisema kuwa amejipanga vizuri kuhakikisha anafunga mabao ya kutosha katika mchezo wa leokwa lengo la kutaka kuendeleza rekodi yake ya mabao.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com