Simba VS Yanga , nani kupata matokeo mazuri leo ?


ILIKUWA mwezi, wiki, siku na sasa zimebaki saa kumalizika kwa ile hadithi tamu inayohusu miamba ya soka nchini, Yanga na Simba.

Timu hizo zinaumana leo kuanzia saa 10 alasiri Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mchezo wa raundi ya 20 ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikishirikisha timu 16.

Filimbi ya kumaliza mpira itakayopulizwa na mwamuzi Jonensia Rukyaa baada ya dakika 90 za waungwana hao kumenyana, ndipo kila upande utakapojua ulichovuna na tambo za mashabiki, wachezaji na viongozi zitakuwa zimeishia hapo.

Simba-VS-Yanga-matokeo-ligi-kuu-bongosoka

Ni mchezo ambao huvuta hisia za mashabiki wengi wa soka, ambao huwa hautabiriki hata kama moja kati ya timu hizo inaonekana uwezo wake ni mdogo kulinganisha na nyingine.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo cha mabao 2-0 ilichokipata Septemba 25 mwaka jana katika mchezo wa duru la kwanza la ligi hiyo, matokeo ambayo bado yanaitesa klabu hiyo.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Amis Tambwe na Malimi Busungu, ambayo kwa kiasi fulani yalipokewa kwa furaha kubwa na mashabiki wa Yanga. Yanga inaingia ikiwa na safu inayotisha ya ushambuliaji ikiongozwa na Mrundi Amis Tambwe anayeshika nafasi ya pili kwa ufungaji akiwa na mabao 14 nyuma ya Hamisi Kiiza wa Simba mwenye mabao 16.

Pia Yanga inaye mshambuliaji raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma, ambaye ameonekana kuwa mwiba mchungu kwa mabeki na raia wa Niger, Issoufou Boubacar. Washambuliaji wengine wa Yanga ni wazawa Simon Msuva, Malimi Busungu, Deus Kaseke na Paul Nonga wanaweza kuwa msaada mkubwa kwa Yanga leo.

Safu ya ushambuliaji ya Simba itakuwa na Kiiza raia wa Uganda, ambaye ni tumaini la timu hiyo katika kucheka na nyavu, akisaidiana na Mzawa, Ibrahim Ajib aliyefunga mabao manane hadi sasa.

Washambuliaji wengine wa Simba ni Danny Lyanga, Haji Ugando na huenda Mussa Mgosi naye akapewa nafasi kutokana na uzoefu wake katika mechi hizo, ingawa amekuwa hana nafasi katika kikosi cha Simba.

Kivutio kikubwa leo itakuwa katika safu ya kiungo, ambapo Yanga inao Thabani Kamusoko na Haruna Niyonzima, Salum Telela na Said Makapu wakati Simba inao Jonas Mkude, Justice Majabvi, Mwinyi Kazimoto na Said Ndemla.

Simba inajivunia safu imara ya ulinzi, ambapo itakuwa na Juuko Murshid na Hassan Isihaka, wakati pembeni inao Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Hassan Ramadhan ‘Kessy’ watakaokuwa na jukumu la kumlinda kipa wao Vincent Angban.

Yanga yenyewe safu yake ya ulinzi kidogo imetetereka kutokana na kuwa majeruhi kwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kufungiwa kwa Kelvin Yondani wote wakiwa walinzi wa kati.

Hata hivyo, bado Yanga ipo imara zaidi, ambapo itawategemea beki Mtogo, Vincent Bossue na Mbuyu Twite wakati pembeni itakuwa na Haji Mwinyi na Juma Abdul kwa ajili ya kumlinda kipa Ally Mustapha ‘Barthez’.

Simba itaingia uwanjani ikiwa chini ya kocha Jackson Mayanja ambaye ameiongoza timu hiyo mechi saba na kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na kuongoza ligi ikiwa na pointi 45, wakati Yanga inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 43. Mazingira ya kuongoza ligi pamoja na kushinda mechi karibu saba mfululizo kwa kiasi fulani yamewapa

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com