Simba watolewa Mapinduzi Cup , wapingwa goli moja na Mtibwa nusu fainali…


Goli la kiungo ambaye soka lake almanusura likatishwe  na Azam FC baada ya kudai ana matatizo ambayo yangemletea madhara kama angeendelea kucheza mpira wakati anaitumikia Azam FC ,  Ibrahim Rajab Jeba limeiondosha  Simba katika michuano ya Mapinduzi cup baada ya timu yake ya Mtibwa Sugar kuwafunga Simba  goli 1 bila majibu.

Katika mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza uliochezwa katika uwanja wa Amani  , mchezo ulianza taratibu kila mmoja akijaribu kujihami na kuweka chini mpira.


Mpaka dakika 15 za kwanza zinakatika hakuna kipa aliyokuwa amepata kuokoa mpira wowote mkali langoni mwao, kitendo kilichotokana na mchezo muda mwingi kuchezwa eneo la kati ya uwanja.

Mtibwa sugar ndio waliokuwa wa mwanzo kufika langoni mwa wapinzani wao lakini walishindwa kutumia nafasi walizotengeneza wakati simba sc wakikosa mbinu ya kupenya ukuta wa Mtibwa sugar.

Dakika ya 45 shuti kali la Ramadhani Shiiza Kichuya lilishindwa kudakwa na mlinda lango wa Simba,  Peter Manyika na unamkuta Ibrahim Jeba na kuiandikia Mtibwa goli la kuongoza na kupeleka mchezo huo mapumziko Mtibwa sugar wakiwa mbele kwa goli 1-0.

Ibrahim-Jeba-Mtibwa-Sugar

Kipindi cha pili Simba SC walianza kwa kufanya mabadiliko ya kumuingiza Ibrahim Ajibu, Brian Majegwa na Said Ndemla kuchukuwa nafasi ya Awadhi Juma, Nimubona na Mussa Mgosi.

Mabadiliko hayo yalirejesha kujiamini kwa simba sc katika eneo la kati na kujaribu kutengeneza nafasi kadha ambazo walishindwa kuzitumia na kupelekea mchezo kumalizika kwa Mtibwa sugar kuibuka na ushindi wa goli 1-0 na kutinga fainali.

Nusu Fainali ya pili ni  kati ya yanga na URA huku mchezo wa fainali ukitarajiwa kuchezwa siku ya jumanne januari 12.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com