Simba ya mwendokasi , Yaitandika Mbao FC 1 – 0 ….


Klabu ya wekundi wa msimbazi , Simba imeendeleza spidi 120 katika kuhakikisha wananyakua ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu baada ya kuibuka na ushindi mfinyu wa goli 1  – 0 dhidi ya timu ngumu wa Mbao FC kwenye mchezo uliopigwa  kwenye uwanja wa Uhuru , Dar-es-salaam .

Goli pekee la Simba lilifungwa na Mzamiru Yassin dakika ya 86 baada ya kumiliki vizuri pasi ya kichwa ya Frederic Blagnon na kupiga shuti kali lililojaa wavuni  na kuipa Simba pointi tatu muhimu.

simba-vs-kagera-sugar-juuko

Katika mchezo wa leo , Simba iliweza kuutawala mchezo huku ikitengeneza nafasi nyingi za mabao lakini sifa ziwaendee mabeki wa mbao FC kwa kazi ya ziada waliyoifanya kuidhibiti  safu ya ushambuliaji ya Simba .

Kwa matokeo hayo Simba inafikisha pointi 26 na kuendelea kujitanua kileleni kwa tofauti ya pointi 6.

Kikosi cha Simba: Vincent Angban, Janvier Bokungu, Mohamed Hussein, Murshid Juuko, Jonas Mkude, Method Mwanjale, Shiza Ramadhani, Mzamiru Yassin, Laudit Mavugo, Ibrahim Hajib, Mwinyi Kazimoto.

Mbao: Emmanuel Mseja, Steve Mganya, Steve Kigoha, Asante Kwasi, Pius Buswita, Youssouf Ndikumana, Robert Magadula, Salmin Hoza, Emmanuel Mvuyekure, Hussein Swedy, Dickson Ambundo.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com