Simba yafunga usajili dirisha dogo


SIMBA imekamilisha usajili wa dirisha dogo baada ya kufikia uamuzi wa kumsajili straika mwenye uwezo wa hali ya juu zaidi ya nyota wa Vital’O ya Burundi, Laudit Mavugo pamoja na kumrejesha kundini mshambuliaji wao waliyemtoa kwa mkopo kwa timu ya KCB ya Kenya, Paul Kiongera.

simba-vs-mgambo-jkt

Sambamba na hilo, Wekundu wa Msimbazi hao wamepata beki king’ang’anizi kutoka moja ya timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, ili kutoa nafasi kwa mchezaji wao wa safu ya ulinzi ambaye wamemwelezea kama kigeugeu na mwenye tamaa ya fedha ambaye hata hivyo jina lake hawakulitaja kuondoka katika klabu hiyo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, straika huyo anayetarajiwa kutua Msimbazi muda wowote kuanzia sasa, ana uwezo wa hali ya juu wa kucheka na nyavu, lakini pia akiwa ni mchezeshaji mzuri wa wenzake, hali inayoweza kuifanya timu yao kuwa moto wa kuotea mbali katika mechi zijazo za Ligi Kuu Bara.

Alisema straika huyo atafahamika baada ya kufika nchini tayari kumalizana na klabu yao na aliwataka mashabiki wa klabu hiyo kutokuwa na wasiwasi juu ya kikosi chao.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com