Simba yaichapa Mtibwa Sugar 2 – 0


Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba , leo wameendeleza dozi baada ya kuifunga Mtibwa sugar mabao 2 – 0  katika mwendelezo wa mzunguko wa nne wa ligi kuu Tanzania bara .

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika , hakuna timu iliyokua imeona lango la mwenzake . Kipindi cha pili , Ibrahim Ajib aliweza kufungua akaunti ya magoli katika dakika ya 52 baada ya kumalizia kwa kichwa pasi nzuri aliyotengenezewa na  Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ .

ibrahim-ajib-simba-vs-mtibwa

Dakika ya 66 , Mshambuliaji  wa simba , Laudit Mavugo  aliweza kufunga bao zuri akiwa ndani ya boksi baada ya pasi ya kiungo Mwinyi Kazimoto.

Ushindi wa Simba katika mchezo huo umeiwezesha Simba kufikisha alama 10 ikiwa imeshacheza michezo minne na kushika nafasi ya pili katika msimamo wa VPL, ikiwa nyuma ya Azam ambayo wanapishana magoli ya kufunga na kufungwa.

Katika mchezo mwingine wa ligi kuu Tanzania bara uliopigwa mbeya ,timu ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa goli moja kwa bila, ushindi huo umeiwezesha Prisons kupanda hadi nafasi ya sita ikiwa na alama saba katika michezo minne.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com