Simba yaichapa Njombe mji na kuiacha Yanga…


Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba , Jana illiweza kuwaacha mahasimu wenzao , Yanga kwa pointi 3 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuitundika klabu ya Njombe Mji mabao 2- 0 katika mechi ya kiporo iliyopigwa kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe .

Magoli yote ya Simba yalifungwa na mshambuliaji wao hatari , John Bocco ambapo dakika ya 17 aliachia shuti kali lililotinga moja kwamoja wavuni na kmuacha kipa wa Njombe mji bila la kufanya .

Bocco aliongeza goli la pili kipindi cha pili cha mchezo katika dakika ya 64 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Shomari Kapombe na kuuweka mpira moja kwa moja wavuni .

Kwa ushindi walioupata Simba , wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 49 nyuma ya Yanga yenye pointi 46 huku timu zote zikiwa na michezo sawa kwasasa .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Bonyeza hapa kupata offer kabampe. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com