Simba yaichapa Yanga , kuubeba ubingwa kwa hesabu hizi…


Klabu ya wekundu wa Msimbazi , Simba leo wameweza kupiga hatua nyingine mbele katika mbio za ubingwa wa ligi Tanzania bara , baada ya kuwafunga watani wao wa Jadi , Klabu ya Yanga goli 1 – 0 katika mchezo wa mwendelezo wa ligi hiyo inayoelekea ukingoni .

Bao pekee la mchezo liliwekwa wavuni na Erasto Nyoni dakika ya 37 ya mchezo akimalizia kwa uzuri kabisa mpira wa adhabu uliopigwa na Shiza Kichuya .

Yanga walicheza karibia kipindi chote cha pili wakiwa pungufu uwanjani baada ya beki wao wa kulia , Hassan  Kessy kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 48 ya mchezo kwa kumchezea rafu beki wa simba ,  Asante Kwasi.

Licha ya kadi nyekundu hio , awali nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani naye alinusurika kupata kadi nyekundu kutokana na kitendo chake cha kumtemea mate beki wa Simba, Kwasi, lakini mwamuzi hakuona tukio hilo pamoja na Mghana huyo kumlalamikia.

Mchezo wa leo ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na Simba ambayo iliweza kupata  kona 8, wakati Yanga ikiweka rekodi ya kucheza dakika 90, bila ya kupiga kona yoyote katika mchezo wa watani wa jadi.

Ushindi walioupata Simba leo unawafanya   kufikisha pointi 62 ikiwa imeshacheza mechi 26 huku wakihitaji pointi 5  tu katika mechi zake 4 zijazo ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano ya kusubili ubingwa huo tokea walipoutwaa mwaka 2012 .

Hesabu ya ubingwa wa simba inaweza ikawa rahisi zaidi kama Yanga yenye pointi 48 huku ikiwa imeshacheza mechi 24 ikipoteza tena mechi  zake 2  zijazo.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com