Simba yaongelea usajili wa Haruna Niyonzima …


Mtandao wa MillardAyo umeripoti taarifa za uwezekano wa klabu ya simba kumsajili Kiungo wa kimataifa wa Yanga , Haruna Niyonzima baada ya siku moja tu kabla kutupiwa virago na klabu yake ya Yanga .

Baada ya taarifa kuanza kuzagaa kuhusu Niyonzima kutua Simba , mtandao huo ulimtafuta afisa habari wa klabu hiyo , Haji manara ambae alikua na haya ya kusema kuhusu tetesi hizo..

Haruna-Niyonzima-Yanga-Bongosoka
“Haruna Niyonzima ukiniuliza mimi hata viongozi wa Simba wanajua kuwa mimi nampenda sana Haruna Niyonzima ila ni mimi Haji Manara, ndio aina ya viungo ninaopenda wawe vile, lazima niseme nampenda lakini mimi sisajilii kazi yangu ni kupewa habari na kuja kuwaambia lakini sijapewa habari za Niyonzima” alisema Manara

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com