Simba yapokea kichapo kutoka kwa mwadui


Klabu ya wekundi wa Msimbazi , Simba , leo wamepoteza mchezo wao wa kwanza katika Ligi Kuu msimu wa 2019/2020 dhidi ya Mwadui FC baada ya kukubali kichapo cha bao 1 – 0 .

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la CCM Kirumba jijini Shinyanga , goli pekee la mchezo lilifungwa na Gerald Mdamu dakika ya 33 ya mchezo baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya beki wa kushoto Khalfan Mbaruku.

Ushindi wa Mwadui umeweza kuharibu rekodi ya Simba ya kutokufungwa katika michezo sita zilizopita za Ligi Kuu.

Kwa matokeo ya leo , Simba inaendelea kuwa kileleni mwa ligi kuu kwa kuwa na point 18 .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com