Simba yatoa kipigo kwa Chipukizi , Tazama goli zote…


Klabu ya wekundu wa msimbazi Simba imeanza kwa kasi katika michuano ya kombe la mapinduzi kwa kuitandika Chipukizi mabao 4 – 1 katika mchezo wa kundi A uliopigwa katika uwanja wa Amaan , Zanzibar .

Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere dakika ya 33 na 59 , Nicholas Gyan dakika ya 56 na John Bocco dakika ya 83 huku bao la pekee la chipukizi likiwekwa wavuni na Evidence Kilongozi dakika ya 55 .

Simba SC watarudi dimbani tena Jumapili kuvaana na KMKM na kumalizia na Mlandege Januari 8, mechi zote zikanzia Saa 2:15 usiku.


Baada ya hapo, kikosi cha Simba SC kitasafiri kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wake wa kwanza wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria Januari 12 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com