Simba yawaduwaza Mbao FC kwa kichapo cha ghafla , yarudi kileleni mwa ligi kuu…


Klabu wa wekundu wa Msimbazi , Simba , leo jioni wameweza kuwaacha mashabiki wa soka la bongo midomo wazi baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3 – 2 dhidi ya mbao FC , iliyokua ikiongoza kwa bao 2 – 0 hadi kipindi cha kwanza kinamalizika .

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya vodacom , Tanzania Bara uliopigwa katika uwanja wa  CCM Kirumba mkoani Mwanza , wenyeji , Mbao FC hawakuweza kuamini kilichotokea kuanzia dakika ya 82 ya   mchezo kipindi cha pili baada ya kuruhusu goli 3 wavuni .

Mbao FC  ndio walikua wa kwanza kuandika bao  ambapo goli la kwanza lilifungwa dakika ya 18 na Sangija huku dakika ya 33 ya mchezo , Benard akiiandikia bao la pili . Hadi kipenga cha kumaliza kipindi cha kwanza kinapulizwa Mbao FC walikua wakiongoza kwa goli 2 – 0 huku wakiwa tayari na matumaini ya kuondoka na pointi 3 muhimu.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi , huku Simba wakianza harakati za kutafuta mabao ya kuzawazisha . Mbao FC walijitahidi kulilinda lango lao lakini ilipofika Dakika ya 80 ya mchezo ,  Kocha mkuu wa simba , Joseph Omog alifanya mabadiliko kwa  kumtoa Pastory Athanas na nafasi yake kuchuliwa na Said Ndemla huku Blagnon na Mavugo wakiingia kuchukua nafasi za Liuzio na Hamad  .

Mabadiliko hayo ndiyo yaliyoweza kuipa Simba nguvu huku mnamo dakika ya 82 ya mchezo , Frederick Blagnon aliweza kuandika bao la kwanza  .

Simba waliendelea kulitafuta goli la kuzawasisha hadi dakika 90 zilipotimia ambapo katika dakikaya 91 , Blagnon aliweza kuipatia bao la kusawazisha Simba kutokana na uzembe wa  golikipa wa Mbao Erick Ngwegwe ambaye aliuacha mpira udunde kisha akashindwa kuudaka kwa usahihi .

Hadi dakika ya 1 ya nyongeza , Mbao FC 2 – 2 2 Simba huku kila mtu akishajiwekea kwamba mpira utaisha kwa sare . Hiyo haikua kama mashabiki wengi walivyotegemea kwani katika dakika ya 90 + 7 , Mzamiru Yassin aliweza kufufua matumaini ya Simba ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu baada ya kupiga  shuti kali  lililomshinda mlinda mlango wa Mbao na kuifanya Simba kuibuka na ushindi wa goli 3 -2 hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa .

Ushindi wa leo unaifanya Simba ipande hadi kileleni mwa ligi kuu ikiwa na pointi 58 na mechi 26 ilizocheza  huku ikiwashusha watani wao wa Jadi ,  Yanga  ambao bado wana mechi moja mkononi .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com