Singida United yaiondosha Yanga kombe la FA


Klabu ya Singida imeungana na Stand United, Mtibwa Sugar na JKT Tanzania kucheza hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA baada ya kuiondosha klabu ya Yanga  kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida .

Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 23 lililofungwa kwa kichwa na Yusuph Mhilu akiunganisha kona iliyopigwa na Ibrahim Ajibu akiwazidi ujanja mabeki wa Singida United.

Singida United ilisawazisha bao hilo dakika ya 46 kupitia kwa Kenny Ally baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Yanga.

Papy Tshishimbi na Gadiel Michael ndio wachezaji wa Yanga waliokosa penalti kwenye mchezo huo na kufanya Yanga iondoshwe kwenye mashindano hayo ambayo klabu hiyo inakumbuka mara ya mwisho kubeba taji hili mwaka 2016 kwa kuifunga Azam kwenye mchezo wa fainali.

Penati za Singida United zilifungwa na Batambuze, Kutinyu, Kenny na Sumbi lakini Antiri mkwaju wake uliokolewa na golikipa wa Yanga Youthe Rostand. Hii inakua ni mara ya kwanza kwa Singida United kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano .

Mashabiki waliofurika kwenye Uwanja wa Namfua walilazimika kufuatilia mechi hiyo huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha hasa kipindi cha kwanza.

Singida itavaana na JKT Tanza­nia kwenye Uwanja wa Namfua, wakati Mtibwa itaumana na Stand United kwenye Uwanja wa Manungu.

Yanga sasa inarejea kujiandaa na mchezo wake wa kuwania ku­fuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi wiki hii dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

 

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Bonyeza hapa kupata offer kabampe. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com