Taifa Stars VS Sudan , Unayopaswa kujua kuelekea CHAN 2020


Timu ya taifa ya Tanzania , Taifa Stars itashuka dimbani leo majira ya saa 1 usiku kuchuana na Sudan katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Cameroon mwaka kesho .

Mshindi wa jumla baina ya timu hizi mbili atapata tiketi ya moja kwa moja kushiriki fainali hizi ambapo mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa October 18 nchini Sudan .

Taifa starts ilifuzu michuano hii kwa mara ya kwanza mwaka 2009 ambapo iliishia hatua ya makundi na tokea hapo haijawahi kushiriki tena huku Sudani ikishiriki mara mbili na mara zote kufanikiwa kutwaa medali ya Shaba kwa kushika nafasi ya tatu mwaka 2011 na mwaka 2019 .

Rekodi nzuri ya Sudan katika michuano hii itakua changamoto kubwa kwa Taifa stars lakini Stars wamejipanga vyakutosha kuwakabili wapinzani wao huku wakihimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi kuishangilia .

“Haitakuwa mechi rahisi kwani ni hatua ya mwisho kuelekea Chan hivyo lazima kila timu itataka kupata matokeo mazuri. Tumejiandaa kupata matokeo mazuri na kutumia vizuri uwanja wa nyumbani kwa kupata ushindi,” alisema Kipa Juma Kaseja katika mahojiano na wandishi wa habari .

Kikosi cha Stars kilichoitwa ni pamoja na

Makipa : Juma  Kaseja, Metacha Mnata, and Saidi Kipao.

Mabeki: Haruna Shamte, Gadiel Michael, Mohammed Hussein, Boniface Maganga, Kelvin Yondani, Idd Mobby and Erasto Nyoni

Viungo : Jonas Mkude, Baraka Majogoro, AbubakarSalum, Frank Domayo, AbdulaziziMakame, Hassan Dilunga, Feisal Salum, MudhatjirYahya, MzamiruYasin, and Mohammed Banka.

Washambuliaji : Ayoub Lyanga, MirajAthumani, and Shaaban Idd Chilunda.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com