Taifa Stars yaitandika Somalia goli 4


Timu ya soka ya taifa ya Tanzania bara the Kilimanjaro Stars jana imefanikiwa kufuta machozi ya kipigo cha bao 7-0 walichokipata dhidi ya Algeria mara baada yakufanikiwa kuwachabanga Wasomalia kwa jumla ya mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza wa kundi A wa fainali za kombe la Challenge uliopigwa katika uwanja wa taifa huko Adis Ababa nchini Ethiopia.
Kikosi-cha-Taifa-Stars
Stars ambayo katika mchezo wa hii leo iling’ara vilivyo huku ikiongozwa na washambuliaji hatari wa timu hiyo Elius Maguli na nahodha wao John Boko waliweza kutawala sehemu kubwa ya mchezo huo na hivyo kufufua matumaini ya kuwa inaweza kufika mbali katika michuano hiyo mikubwa kwa ukanda huu wa CECAFA kwa ngazi ya timu za taifa.
Bocco na Maguli walifunga magoli yote manne huku kila mmoja akifunga moja katika kila kipindi baada ya kili stars kupata magoli mawili kwa kila kipindi nakukamilisha kipigo kama ambacho Barcelona iliipa Real Madrid jana katika La Liga Uwanja wa Bernabeu.
Kipa Aishi Manula aliyeanza leo alifanya kazi nzuri ya kuokoa michomo mingi ya hatari langoni mwake na kujizolea sifa kemkem.
Matokeo hayo, yanaifanya Kili Stars inayofundishwa na mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ ianzie kileleni mwa Kundi A ikiwashusha Rwanda walioifunga Ethiopia 1-0 jana.
Katika mchezo huo ambao Tanzania Bara kilimanjaro stars iling’ara vilivyo iliwakilishwa na kikosi kifuatacho:
golini alikuwa ; Aishi Manula, mabeki wa pembeni- Shomary Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, mabeki wa kati- Kevin Yondan, Salum Mbonde, viungo wa kati na pembeni ni – Himid Mao, Simon Msuva/Malimi Busungu dk71, Said Ndemla, na washambuliaji ni- Johm Bocco, Elias Maguli na Deus Kaseke.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com