Tanzania Vs Kenya Afcon takwimu zinasemaje?


Wakati Tanzania (Taifa Stars) ikitarajiwa kuingia uwanjani leo kukabiliana na majirani zao Kenya (Harambee Stars) kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Michuano ya Afcon inayoendelea nchini Misri , macho na masikio ya mashabiki wa soka Afrika Mashariki yanasubiri kwa hamu kuona nani ataibuka mshindi kwenye mchezo utakaopigwa majira ya saa 5 za usiku saa za Afrika Mashariki . Lakini je Takwimu zinasemaje ?

  • Tanzania na Kenya wamekutana mara 44 huku Kenya wakishinda michezo 20, draw 14 and Tanzania wakishinda michezo 14 . .
  • Katika Michezo Sita ya mwishi Tanzania Wameshinda 1 , Wamepoteza 3 na Ku-draw 2 huku Kenya wakishinda 2 , kupoteza 3 na draw 1 .
  • Katika Mchezo wa Ufunguzi timu zote mbili zilimaliza mchezo bila ya kupiga shuti hata moja golini (Shot on target) lakini katika mchezo wa leo tutegemee mashambulizi kwa pande zote mbili .
  • Tanzania inarejea katika michuano ya Afcon baada ya miaka 39 huku kwa upande wa Kenya imepita miaka 15 . Timu zote zitakua na kiu ya kuweka historia baada ya miaka mingi kukosekana kwenye mashindano hivyo mchezo wa leo utakua ni kufa na kupona kwani atakayefungwa atayaaga mashindano .

Mechi zao za Kwanza Afcon

Tanzania (Taifa Stars)

  • Taifa Stars haikutegemewa kuwafunga Senegal , moja ya timu zinazotajwa kuchukua kombe la Afcom mwaka huu .
  • Katika Mchezo wa Tanzania na Senegal ulioisha kwa goli 2 – 0 , Tanzania hawakuweza kulisumbua goli la Senegal hata mara moja .
  • Kocha wa Tanzania , Emmanuel Amunike alisema kuwa katika mechi ya kwanza dhidi ya Senegal wachezaje wake walikua na hofu ya mchezo na kitendo cha kumtoa  Feisal Salum Abdalla kipindi cha kwanza kilionyesha mabadiliko.

Kenya (Harambee Stars)

  • Kenya nao pia walishindwa kufanya shambulizi lotote (Shot on Target) dhidi ya Algeria kwahiyo inabidi wautumie mchezo wa leo kuonyesha uwezo wao kama wanataka kusonga mbele .
  • Baada ya kufungwa goli 2 – 0 kipindi cha Kwanza, tayari mchezo ulikua kama umeisha kwani hakuna mengi yaliyoendelea kipindi cha pili .

Je , Nani kuibuka Mshindi ?

Inaonekana kuna uwezekano mkubwa kwa mchezo huu kuisha kwa draw .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com