Tanzania yachapwa 3 – 0 na Cape Verde kufuzu AFCON


Kikosi cha Timu ya taifa ya Tanzania , Taifa Starts kimeweza kupoteza mchezo wake wa kufuzu fainali za AFCON dhidi ya Cape Verde baada ya kukubali kichapo cha goli 3 – 0 katika mchezo uliopigwa katika  uwanja wao wa Taifa  jijini Praia  saa 2:00 usiku.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Cape Verde ilikua ikiongoza kwa goli 2 – 0 , goli zilizofungwa na Ricardo Gomez katika dakika ya 16 na 23 ya mchezo .

kocha wa Taifa Starts  alifanya mabadiliko dakika ya 38 ya mchezo kwa  kumtoa Gadiel Michael na kumuingiza  Shomari Kapombe .

Dakika ya 80 ya mchezo , mshambuliaji John Bocco aliingia na kuweza angalau kusumbua safu ya ulinzi ya Cape Verde huku moja ya nafasi alizopoteza ikiwa ni mpira wa kichwa uliogongwa mwamba .

Dakika ya 85 ya mchezo , Ianique Taraves aliweza kuihakikishia ushimdi Cape Verde baada ya kupigilia msumari wa mwisho wa ushindi na hadi kipenga cha mwisho Cape Verde 3 Taifa Starts ikitoka bila kitu .

Mchezo wa marudiano utapigwa Oktoba 16 katika uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam .

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com