Tetesi: Arsenal kutema watano, Ronaldo sasa ni Man Utd au PSG…


Ligi mbalimbali duniani, zimesimama kutokana na madhara yanayoendelea kuzikumba nchi mbalimbali duniani kutokana na usambaaji wa virusi vya Corona, ugonjwa ujulikanao kama Covid-19.

Lakini huku kukiwa na imani ya hali kurejea kuwa shwari baada ya janga hili, timu mbalimbali zinaendelea na harakati za kusuka mipango ili kuwa imara zaidi hali itakaporejea kuwa sawa tena.

Vyanzo mbalimbali vya habari barani Ulaya, vinaendelea kuripoti tetesi za usajili kwa timu hizo.

Kikosi cha Arsenal msimu wa 2019/20.

Arsenal kutema watano (5)…

Klabu ya soka ya Arsenal, imejipanga kuendelea kupunguza wachezaji ambao hawana msaada katika timu hiyo, ikiwa ni njia ya kurejea katika ushindani.

Imeripotiwa kuwa kocha wa washika bunduki hao wa London, Mikel Arteta atapunguza wachezaji watano katika hatua ya kwanza, huku waliotajwa katika orodha hiyo wakiwa ni Shkodrani Mustafi, Sokratis Papastathopoulos, Saed Kolasinac, Henrik Mkhitaryan na Mohamed Elneny – Mirror.

Cristiano Ronaldo

Ronaldo kutimka Juve…

Imeripotiwa kuwa mshambuiliaji Cristiano Ronaldo anataka kuondoka Juventus, huku akihusishwa zaidi na kurejea Manchester United au Kuelekea Ufaransa kujiunga na Paris Saint-German.

Ronaldo anatajwa kuwa na ofa kutoka kwa matajiri hao wa jiji la Paris, huku ikiwa ni kiu ya matajiri hao, kutengeneza pea ya mshindi mara tano wa Ballon D’ Or pamoja na Kylian Mbappe, ambaye anaonekana kuwa mchezaji bora zaidi kijana kwa sasa.

Nyota huyo wa Ureno pia amepokea ombi kutoka kwa klabu yake ya zamani ya Man United na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 anataka kurejesha ufalme wake pale Old Trafford, ingawa inategemea kama United itafuzu ligi ya mabingwa – Diario Gol.

Antoine Griezmann

Griezman kuondoka Barca, Neymar ndani…

Imeripotiwa kuwa mabingwa wa soka la nchini Hispania, klabu ya soka ya Barcelona imepanga kumuuza mshambuliaji wake Antoine Griezmann katika majira ya kiangazi, baada ya kushindwakuonyesha makali ndani ya Nou Camp.

Griezmann akifunga mabao 14 na kutoa assist 4 ndani ya mechi 37, huku akishindwa kufikia matarajio ndani ya klabu, thamani yake inatajwa kuwa ni Euro Milioni 100.

Tetesi za kuondoka kwa Griezman ndani ya Barcelona ni ishara nzuri kwa nyota wa zamani watimu hiyo, mbrazil Neymar jr ambaye pia ametajwa kuwa na shauku ya kuondoka Paris Saint-Germain na kurejea Hispania kuitumikia miamba hiyo ya Catalunya.

Fabian Ruiz, SSC Napoli

Liverpool kuibomoa Napoli…

Kiungo wa kati wa klabu ya Napoli, Fabian Ruiz anatajwa kuwaniwa kwa karibu na mabingwa wa soka barani Ulaya, Liverpool kwenye dirisha la uhamisho la majira ya kiangazi.

Imeripotiwa kuwa vinara hao wa ligi kuu ya England, Liverpool wako tayari kulipa ada ya uhamisho inayotajwa kuwa ni takribani paundi milioni 78 kwa ajili ya Fabian.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Hispania, anatajwa kuwindwa pia na miamba ya soka ya nchini humo, Real Madrid na Barcelona.

Mario Gotze.

Gotze na Dortmund kubwagana…

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya soka ya Borussia Dortmund, Mario Gotze ameripotiwa kugoma kusaini mkataba mpya na klabu hiyo huku akitaka kuondoka majira ya kiangazi baada ya kukataa kipengele cha kupunguziwa mshahara katika mkataba wake mpya.

Ripoti zinasema pande zote mbili zimeshindwa kuafikiana juu ya punguzo hilo la mshahara, linalotajwa kushuka kwa aslimia 20 (-20%) kutoka paundi milioni 9 mpaka paundi milioni 7.2.

Gotze ambaye mwaka 2014, alijizolea umaarufu mkubwa hasa baada ya kufunga bao katika mchezo wa fainali za kombe la Dunia dhdidi ya Argentina, kule nchini Brazil, mkataba wake wa sasa unamalizika Juni 30.

Tayari klabu za Hertha Berlin na Inter Milan, zimeonesha nia ya kuhitaji huduma ya mchezaji huyo wa kijerumani mwenye umri wa miaka 27.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com