TImu zinazoongoza kufunga na kufungwa ligi kuu Tanzania Bara..


LICHA ya mashabiki wa Simba kulalamikia kikosi chao kukosa ubingwa msimu huu na kuiachia Yanga, kwa upande mwingine safu yao ya ulinzi inastahili pongezi kwani  ndiyo iliyofungwa mabao machache zaidi.

Ukuta huo wa Simba ambao unaongozwa na Mganda Jjuuko Murshid, umeachia wavu wake utikiswe mara 15, wakati Yanga imetunguliwa mabao 18.

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 62, nyuma ya Azam FC yenye pointi 63 na Yanga ambao tayari wametangazwa mabingwa wa msimu huu baada ya kufikisha pointi 72.

Kikosi-cha-Simba-SC

Lakini Simba licha ya kutotwaa taji hilo kwa msimu wa tatu sasa inajivunia kumiliki ukuta ulio mgumu zaidi ambao umeruhusu mabao machache kuliko timu nyingine 15 zinazoshiriki ligi hiyo.

Wakati Simba ikijivunia kuwa na  ukuta imara, Yanga ina jeuri kwa upande wa safu ya ushambuliaji, huku African Sports ikiweka rekodi ya kuwa na safu butu zaidi ya ushambuliaji.

Kikosi cha Yanga

Safu ya ushambuliaji ya Yanga inayoongozwa na Donald Ngoma imefunga mabao 68, huku safu ya ushambuliaji ya African Sports ambayo ndiyo mbovu kabisa ikifunga mabao 13 peke yake.

Kwa upande wa Coastal Union ambayo imeshashuka daraja safu yao ya ulinzi ndiyo mbovu kabisa sawa na ile ya Toto African, kwani kila moja imekubali kufungwa mabao 39 wakifuatiwa na Majimaji walioruhusu kufungwa mabao 38.

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com