Usajili wa Simba 2019-2020, wachezaji wapya hawa hapa…


Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania bara , Klabu ya wekundu wa Msimbazi , Msimu wa 2019-2020 wamejipanga vyema kuhakikisha wanatetea taji hilo kwa kufanya usajili wa nguvu kwa ajili ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi hapo agosti 23 mwaka huu .

Simba wamesajili wachezaji wapya 11 kama ifuatavyo : –

1 . Miraji Athumani (Lipuli – Iringa)

Huyu ni Kiungo Mshambuliaji mpya wa Simba aliyesajiliwa kutokea Lipuli FC ya Iringa . Miraji”Shevchenko” anarejea Msimbazi baada ya Misimu mitano tokea aondoke huku akizichezea klabu za Lipuli Fc na Mwadui kabla ya hapa.

2 . Kennedy Juma (Singida United – Singida)

Aliyekua mlinzi wa kati na nahodha wa klabu ya Singida United, Kennedy Juma naye alifanikiwa kumwaga wino kuitumikia Simba kwa mkataba wa miaka miwili .

3 . Tairone da Silva (Atletico Cearense FC – Brazil)

Simba ilifanikiwa pia kumnasa beki Tairone Santos da Silva  (30) kwa kandarasi ya miaka miwili . Tairone Santos da Silva amejiunga na Simba SC akitokea klabu ya Atletico Cearense FC inayocheza Ligi Daraja la Nne nchini Brazil, maarufu kama Serie D.

4 . Gerson Viera (ATK – India)

Huyu ni beki Mbrazil mwenye umri wa miaka 26 ambaye naye alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya wekundu wa msimbazi .

Vieira amewahi kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya wachezaji chini ya miaka 17 ya Brazil iliyokuwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Philippe Coutinho, Casemiro na golikipa Liverpool Alisson Becker.

Nyota huyo pia alicheza timu ya Taifa ya Brazil ya wachezaji chini ya umri wa miaka 20 sambamba na kusakata kabumbu katika vilabu kadhaa nchini humo ikiwepo Grêmio kabla ya kutimkia ATK FC ya India.

5 . Wilker da Silva (Bragantino – Brazil)

Mshambuliaji Wilker Henrique da Silva mwenye umri wa miaka 23, alisaini kandarasi la miaka miwili kukipiga na mabingwa wa Tanzania Bara akitokea klabu ya Bragantino ya Brazil.

Katika takwimu za mwaka 2018 katika ligi ya Paulista A3, Mbrazil huyo alicheza mechi 15 na kufunga mabao mawili ikiwa ni wastani wa bao 0.83 kwa mechi huku akipata kadi za njano tatu na nyekundu moja.

6 . Francis Kahata (Gor Mahia – Kenya)

Huyu ni Kiungo mshambuliaji aliyekua akikipiga katika klabu ya Gor Mahia . Kahata naye alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Simba .

Akiwa kwenye klabu hiyo (Gor Mahia) alishinda Kombe la Ligi Kuu mara tatu, kiungo bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Kenya mara mbili na mchezaji bora wa msimu 2018/2019 wa Gor Mahia

7 . Deo Kanda (TP Mazembe – Congo)

Huyu ni winga wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Deo Gracia Kanda Mukoko ambae naye alimwaga wino kwa mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na wekundu wa msimbazi akitokea TP Mazembe ya Lubumbashi.

8 . Sharaf Shiboub (Al Hilal – Sudan)

Huyu ni Kiungo wa kimataifa wa Sudan, Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman, aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja .

Sharaf Abdalrahman ametua mitaa ya Msimbazi akitokea klabu ya Al Hilal ya nchini Sudan ambayo ameitumikia kwa mafanikio makubwa.

9. Ibrahim Ajibu (Yanga – Dar-es-salaam)

Simba ilifanikiwa kumrejesha aliyekua nyota wake , Ibrahim Ajibu kutoka kwa watani wao wa jadi , Yanga .

Ajibu alisajiliwa kutokea Yanga kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika huku akiweka kandarasi la miaka miwili kuwatumikia wana msimbazi .

10 . Gadiel Michael (Yanga – Dar-es-salaam)

Gadiel Michael na yeye pia aliweza kujiunga na wana msimbazi kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika na Yanga huku akisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba .

11 . Beno Kakolanya (Yanga – Dar-es-salaam)

Aliyekua kipa wa Yanga SC, Beno Kakolanya naye alifanikiwa kuamia upande wa pili baada ya kumwaga wino kuitumikia Simba kwa mkataba wa miaka miwili .

Kwa misimu miwili aliyokaa Yanga, David Kakolanya amedaka mechi 24 tu, kabla ya kujiondoa mwenyewe akiituhumu klabu kukiuka vipengele vya mkataba ambao mwishowe ulivunjwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Bongosoka imeungana na kampuni maarufu ya kubet ya 1XBet , Jiunge Hapa. Tufuate instagram , facebook na twitter. Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com